1 line
632 B
Plaintext
1 line
632 B
Plaintext
\v 15 Wakawakusanya ndugu zao, wakajitakasa wenyewe, na wakaenda ndani, kama alivyoamru mfalme, wakifuata maneno ya Yahwe, kwa ajili ya kuisafisha nyumba ya Yahwe. \v 16 Makuhani wakaenda kwenye sehemu za ndani ya nyumba ya Yahwe kwa ajili ya kuisafisha; wakaleta nje uchafu wote walioukuta ndani ya hekalu la Yahwe katika uwanja wa nyumba. Walawi wakauchukua kuubeba nje ya hadi kwnye kijito cha Kidroni. \v 17 Sasa wakaanza utakaso katika siku ya kwanza ya mwezi. Katika siku ya nane ya mwezi wakaufikia ukumbi wa Yahwe. Kisha siku nane zaidi wakaitakasa nyumba ya Yahwe. Katika siku ya kumi na sita ya mwezi wa kwanza wakamaliza. |