sw_2ch_text_reg/35/07.txt

1 line
639 B
Plaintext

\v 7 Yosia akawapa watu wote wanakondoo elfu thelathini na wanambuzi kutoka katika makundi kwa ajili ya sadaka za Pasaka kwa wote waliokuwepo, na pia akatoa ng'ombe dume elfu tatu; hawa walikuwa kutoka katika mali ya mfalme. \v 8 Viongozi wake wakatoa sadaka za hiari kwa watu, makuhani, na Walawi. Hilki, Zekaria, na Yeieli, viongozi wasimamizi wa nyumba ya Mungu, wakawapa makuhani ndama 2, 600 na ng'ombe mia tatu kwa ajili ya matoleo ya Pasaka. \v 9 Pia Konania, Shemaya na Nethaneli, ndugu zake, na Hashabia, Yeieli, na Yazabadi, mkuu wa Walawi, akawapa Walawi wana-kondoo elfu tano na ng'ombe mia tano kwa ajili ya matoleo ya Pasaka.