sw_2ch_text_reg/34/01.txt

1 line
538 B
Plaintext

\c 34 \v 1 Yosia alikuwa na umri wa miaka nane alipoanza kutawala; alitawala miaka thelathini na moja katika Yerusalemu. \v 2 Alifanya yaliyohaki katika macho ya Yahwe, na alitembea katika njia za Daudi babu yake, na hakugeuka mbali iwe kulia au kushoto. \v 3 Kwa maana ndani ya miaka minane ya ya utawala wake, alipokuwa bado kijana, alianza kumtafuta Mungu wa Daudi, babu yake. Katika miaka ishirini, alianza kuisafisha Yuda na Yerusalemu kutoka sehemu za juu, vituo vya Maashera, na sanamu za kuchonga na sanamu za chuma ya kuyeyushwa.