sw_2ch_text_reg/24/13.txt

1 line
480 B
Plaintext

\v 13 Kwa hiyo wafanya kazi wakafanya kazi, na kazi ya kukarabati ikasonga mbele mikononi mwao; waakaisimamisha nyumba ya Mungu katika hali yake halisi na kuiimarisha. \v 14 Walipomaliza, wakaleta fedha zilizobaki kwa mfalme na Yehoyada. Fedha hizo zilitumika kutengenezea samani kwa ajili ya nyumba ya Yahwe, vyombo vya huduma na kutolea dhabihu—vijiko na vyombo vya dhahabu na fedha. Wakatoa sadaka za kuteketezwa bila kukomaa katika nyumba ya Yahwe kwa siku zote za Yehoyada.