sw_2ch_text_reg/06/26.txt

1 line
395 B
Plaintext

\v 26 Wakati mbingu zimefungwa na hakuna mvua kwa sababu watu wamekutenda dhambi—ikiwa wataomba kuelekea sehemu hii, wakilikili jina lako, na kuziacha dhambi zao utakapokuwa umewaadhibu— \v 27 basi sikia mbinguni na usamehe dhambi za watumishi wako na watu wako Israeli, utakapowaelekeza kwenye njia njema iwapasayo kutembea. Tuma mvua juu ya nchi yako, ambayo umewapa watu wako kama urithi.