sw_2ch_text_reg/09/27.txt

1 line
666 B
Plaintext

\v 27 Mfalme alikuwa na fedha katika Yerusalemu, nyingi kama mawe juu ya aridhi. Akazifanya mbao za mierezi kuwa nyingi kama miti ya mikuyu ambayo iko nyanda za chini. \v 28 Wakaleta farasi kutoka Misri na kutoka nchi zote kwa ajili ya Selemani. \v 29 Kwa mambo mengine kuhusu Selemani, mwanzo na mwisho, hayajandikwa katika Historia ya Nathani Nabii, katika unabii wa Abiya Mshinoni, na katika Maono ya Ido mwonaji wa mambo ya Yeroboamu mwana wa Nabati? \v 30 Selemani akatawala katika Yerusalemu juu ya Israeli yote kwa miaka arobaini. \v 31 Akalala na babu zake na watu wakamzika katika mji wa Daudi baba yake. Rehoboamu, mwanaye, akawa mfalme katika sehemu yake.