sw_2ch_text_reg/09/19.txt

1 line
602 B
Plaintext

\v 19 Simba kumi na wawili walisimama juu ya zile ngazi, mmoja kila upande wa ngazi sita. \v 20 Hapakuwa na kiti cha enzi kama hicho katika ufalme wowote mwingine. Vikombe vyote vya kunywea vya Selemani vilikuwa vya dhahabu, na vikombe vyote vya mfalme katika Nyumba ya Msitu wa Lebanoni vilikuwa vya dhahabu halisi. Hakuna hata kimoja kilichokuwa cha fedha kwa sababu fedha haikuchuliwa kuwa ya thamani katika siku za Selemani. \v 21 Mfalme alikuwa na meli zilizosafiri baharini, pamoja na meli za Hiramu. Mara moja kwa mwaka meli zilileta dhahabu, fedha, na pembe, na manukato, na pia nyani na tausi.