sw_2ch_text_reg/08/16.txt

1 line
464 B
Plaintext

\v 16 Kazi yote aliyoagizwa na Selemani ikakamilika, kutoka siku msingi wa nyumba ya Yahwe ulipowekwa hadi ilipokamilika. Nyumba ya Yahwe ikamalizika. \v 17 Kisha Selemani akaenda Esion geberi, na Elothi, juu ya pwani katika nchi ya Edomu. \v 18 Hiramu akatuma meli zake kupitia watumishi wake ambao walikuwa wana maji wenye uzoefu. Wakasafiri na Selemani na watumishi wa Semani hadi Ofiri. Wakachukua kutoka huko talanta 450 za dhahabu ambazo walimletea Selemani.