sw_2ch_text_reg/07/19.txt

1 line
777 B
Plaintext

\v 19 Lakin ukigeuka, na kuzisahau sheria zangu na amri amabzo nimeweka mbele yenu, na kama utaenda kuabudu miungu wengine na kuwasujudia, \v 20 basi nitawang'oa kutoka kwenye nchi yangu amabayo nimewapa. Nyumba hii ambayo nimeitakasa kwa ajili ya jina langu, nitaitupilia mbali kutoka mbele zangu, na nitaifanya kuwa methali na utani miongini mwa watu wote. \v 21 Ingawa hekalu hili hili zuri sana kwa sasa, kila mtu apitaye karibu yake atashangazwa na ataguna. Watauliza, 'Kwa nini Yahwe ameifanyia hivi nchi hii na nyumba hii', \v 22 wengine watajibu, 'Kwa sababu walimsahau Yahwe, Mungu wao, ambaye alikuwa amewatoa babu zao nje ya nchi ya Misiri, na wakashikamana na miungu wengine na kuwainamia chini na kuwaabudu. Hii ndiyo maana Yahwe ameleta majanga haya yote juu yao"