sw_2ch_text_reg/05/11.txt

1 line
958 B
Plaintext

\v 11 Ilikuwa makuhani walipotoka nje ya sehemu takatifu. Makuhanai wote wliokuwepo wakajiweka wakifu wenyewe kwa Yahwe, bila kujiamuru wenyewe kulingana na sehemu zao. \v 12 Pia makuhani waliokuwa waimbaji, wote kwa ujumla wao, pamoja na Asafu, Hemani, Yeduthuni, na wana wao na ndugu zao, wakiwa wamevalia kitani safi na wakipiga matoazi, vinanda, na vinubi, wakaasimama upande wa mashariki wa mwisho wa madhabahu. Pamoja nao palikuwa na makuhuni 120 wakipuliza tarumbeta. \v 13 Ikawa kwamba wapuruza tarumbeta na waimbaji wakafanya mziki pamoja, wakifanya sauti moja isikike kwa ajili ya kumsifu na kumshukuru Yahwe. Walipaza sauti zao kwa tarumbeta, toazi na vyombo vingine, na wakamsifu Yahwe. Wakaimba, "Kwa maana Yeye ni mwema, kwa kuwa uaminifu wa agano lake wadumu milele." Kisha nyumba, ile nyumba ya Yahwe, ikajawa na wingu. \v 14 Makuhani hawakuweza kusimama ili wahudumu kwa sababu ya lile wingu, kwa maana utukufu wa Yahwe uliijaza nyumba yake.