sw_2ch_text_reg/04/19.txt

1 line
645 B
Plaintext

\v 19 Selemani akazitengeza samani zote ambazo zilikuwa kwenye nyumba ya Mungu, pia madhabahu ya dhahabu, na meza ambazo juu yake mkate wa uwepo ulipaswa kuwekwa; \v 20 vinara pamoja na taa zake, ambazo zilitengezwa ili kumulika mbele ya chumba cha ndani—hivi vilitengenezwa kwa dhahabu halisi; \v 21 na maua, taa, na makoleo, ya dhahabu, dhahabu safi. \v 22 Pia mikasi ya taa, na mabakuli, vijiko, na vikaango vya sadaka za kuteketezwa vyote vilitengenezwa kwa dhahabu safi. Kuhusu mlanago wa kuingilia kwenye nyumba, milango yake ya ndani kwenye patakatifu pa patakatifu na milango ya nyumba, ambayo ni, ya hekalu, ilitengenezwa kwa dhahabu.