sw_2ch_text_reg/02/04.txt

1 line
498 B
Plaintext

\v 4 Tazama, niko karibu kujenga nyumba kwa ajili ya jina la Yahwe Mungu wangu, kuiweka wakifu kwake, kwa ajili ya kumtolea sadaka za kuteketezwa zenye viungo vitamu mbele zake, kwa ajili ya mkate wa uwepo, na kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa asubuhi na jioni, katika siku za Sabato na za mwezi mpya, na katika sikukuu zilizoteuliwa kwa ajili ya Yahwe Mungu wetu. Hii itakuwa milele, kwa Israeli. \v 5 Nyumba nitakayoijenga itakuwa kubwa sana, maana Mungu wetu ni mkuu kuliko miungu mingine yote.