sw_2ch_text_reg/01/14.txt

1 line
669 B
Plaintext

\v 14 Selemani akakusanya magari na wanaume waendesha farasi, naye alikuwa na magari 1, 400 na waendesha farasi kumi na mbili elfu ambao aliwaweka katika miji ya magari, pamoja naye, mfalme katika Yerusalemu. \v 15 Mfalme akatengeneza fedha na dhahabu kuwa vitu vya kawaida kama mawe katika Yerusalemu, na mbao za mierezi kuwa kama miti ya mikuyu iliyomo katika nyanda za chini. \v 16 Selemani katika uagizaji wa farasi kutoka Misiri, wafanya biashara wake walinunua farasi kutoka Misiri kwa bei stahiki. \v 17 Waliagiza gari kutoka Misiri kwa shekeli mia sita za fedha, na farasi mmoja kwa shekeli 150. Pia walinunua kutoka kwa wafalme wa Wahiti na wafalme wa Washamu.