sw_2ch_text_reg/29/22.txt

1 line
608 B
Plaintext

\v 22 Kwa hiyo wakawachinja ng'ombe, na makuhani wakaipokea damu na kuinyunyiza juu ya madhabahu. Wakawachinja kondoo dume, na kunyunyiza damu juu ya madhabahu; Pia wakawachinja wanakondoo na kuinyunyiza damu juu ya madhabahu. \v 23 Wakawaleta mbuzi kwa ajili ya sadka ya dhambi mbele ya mfalme na kusnyiko; wakaweka mikono yao juu ya hao mbuzi. \v 24 Makuhani wakawachinja, na wakafanya sadaka ya dhambi kwa damu yao juu ya madhabahu ili kufanya upatanisho kwa ajili ya Israeli wote, kwa maana mfalme alikuwa ameamuru kuwa sadaka ya kuteketezwa na sadaka ya dhambi lazima zifanywe kwa ajili ya Israeli wote.