sw_2ch_text_reg/06/36.txt

1 line
872 B
Plaintext

\v 36 Kama wametenda dhambi dhidi yako—kwa kuwa hakuna asiye tenda dhambi—na ikiwa una hasira nao na kuwakabidhi kwa adui zao, ili kwamba adui wakawabeba na kuwachukua kama mateka katika nchi zao, iwe mbali au karibu. \v 37 Kisha wakatambua kuwa wako katika nchi ambako wamewekwa utumwani, na ikiwa watatubu na kutafuta msaada kwako katika utumwa wao. Ikiwa watasema, 'Tumetenda kinyume na kutenda dhambi. Tumetenda kwa uovu,' \v 38 ikiwa watarudi kwako kwa mioyo yao yote na kwa nia yao yote katika nchi ya utumwa wao, ambako walichukuliwa kama mateka, na ikiwa wataomba kukabili nchi yao, uliyowapa babu zao, na kukabili mji ambao uliuchagua na kukabili nyumba ambayo niliijenga kwa ajili ya jina lako. \v 39 Basi sika kutoka mbinguni, mahali unapoishi, sikia kuomba kwao na maombi na wayaombayo, na uwasaidie shida zao. Wasamehe watu wako, ambao wamekutenda dhambi.