sw_2ch_text_reg/32/20.txt

1 line
394 B
Plaintext

\v 20 Hezekia, mfalme, na Isaya mwana wa Amozi, nabii, wakaomba kwa sababu ya jambo hili na wakalia hadi mbinguni. \v 21 Yahwe akatuma malaika, ambaye aliwaua wanaume wa kupigana vita, majemedari, na maakida wa mfalme katika kambi. Kwa hiyo Senakeribu akarudi katika nchi yake akiwa na uso wa aibu. Alipokuwa ameenda katika nyumba ya muungu wake, baadhi ya watoto wake wakamuua huko kwa upanga.