sw_2ch_text_reg/06/18.txt

1 line
476 B
Plaintext

\v 18 Lakini kweli Mungu ataishi na wanadamu juu ya dunia? Angalia, dunia yote na mbingu yenyewe haviwezi kukubeba -sembuse na hekalu hili nililojenga! \v 19 Nakusihi yaheshimu maombi haya ya mtumishi wako na ombi lake. Yahwe Mungu wangu; sikia kilio na maombi ambayo mtumishi wako anaomba mbele zako. \v 20 Fumbua macho yako kuelekea hekalu hili usiku na mchana, sehemu ambayo uliahidi kuliweka jina lako. Nakuomba usikie maombi atakayoomba mtumishi wako kuelekea sehemu hii.