sw_2ch_text_reg/07/19.txt

1 line
357 B
Plaintext

\v 19 Lakin ukigeuka, na kuzisahau sheria zangu na amri ambazo nimeweka mbele yenu, na kama utaenda kuabudu miungu wengine na kuwasujudia, \v 20 basi nitawang'oa kutoka kwenye nchi yangu ambayo nimewapa. Nyumba hii ambayo nimeitakasa kwa ajili ya jina langu, nitaitupilia mbali kutoka mbele zangu, na nitaifanya kuwa methali na utani miongini mwa watu wote.