|
\v 15 Waimbaji, wana wa Asafu, walikuwa katika nafasi zao, kama ilivyoagiwa na Daudi, Asafu, Hemani, na Yeduthuni, mwonaji wa mfalme, na walinzi walikuwa katika kila lango. Hawakutakiwa kuziacha huduma zao, kwa sababu ndugu zao Walawi walifanya maandalizi kwa ajili yao. |