1 line
766 B
Plaintext
1 line
766 B
Plaintext
\v 12 Barua kutoka kwa nabii Eliya ikaja kwa Yerohamu. Ilisema, "Hivi ndivyo Yahwe, Mungu wa Daudi, babu yako, anasema: Kwa sababu hujatembea katika njia za Yehoshafafati, baba yako, wala katika njia za Asa, mfalme wa Yuda, \v 13 bali umetembea katika njia za wafalme wa Israeli, na umewafanya Yuda na wakaaji wa Yerusalemu kuenenda kama kahaba, kama nyumba ya Ahabu walivyofanya—na kwa sababu pia umewaua ndugu zako katika familia ya baba yako kwa upanga, watu waliokuwa bora kuliko wewe mwenyewe— \v 14 ona, Yahwe atawapiga watu wako na pigo kubwa, watoto wako, wake zako, na mali zako zote. \v 15 Wewe mwenyewe utakuwa na ugonjwa mwingi kwa sababu ya ugonjwa kataika katika utumbo wako, mpaka utumbo wako uanguke nje kwa sababu ya ugonjwa, siku baada ya siku. |