sw_2ch_text_reg/34/31.txt

1 line
421 B
Plaintext

\v 31 Mfalme akasimama katika sehemu yake na kufanya agano mbele za Yahwe, kutembea mbele za Yahwe, na kuzishika amri zake, taratibu zake, na sheria zake, kwa moyo wake wote na roho yake yote, kuyatii maneno ya agano yaliyokuwa yameandikwa katika kitabu hiki. \v 32 Aliwasababisha wote walioonekana katika Yerusalemu na Benyamini kusimama kwa agano. Wakaaji wa Yerusalemu wakatembea kwa agano la Mungu, Mungu wa babu zao.