sw_2ch_text_reg/34/20.txt

1 line
584 B
Plaintext

\v 20 Mfalme akamwamuru Hilkia, Ahikamu mwana wa Shafani, Abdoni mwana wa Mika, Shafani mwaandishi, na Asaya, mtumishi wake, akisema, \v 21 "Nendeni mkaulize mapenzi ya Yahwe kwa ajili yangu, na kwa wale waliobaki katika Israeli na Yuda, kwa sababu ya maneno ya kitabu ambacho kimeokotwa. Kwa maana ni kuu, ghadhabu zake Yahwe zilizomiminwa juu yetu. Kwa kuwa ni kuu, kwa sababu babu zetu hawakuyasikiliza maneno ya kitabu hiki ili kuyatii yote yaliyokuwa yameandikwa ndani yake". (Badala ya "ambayo yamemiminwa juu yetu", baadhi ya matoleo yanasema " ambayo yamemulikwa dhidi yetu").