sw_2ch_text_reg/34/12.txt

1 line
467 B
Plaintext

\v 12 Watu waliifanya kazi kwa uaminifu. Wasimamizi wao Yahathi na Obadia, Walawi, wa wana wa Merari; na Zekaria na Meshulamu, kutoka kwa wana wa Wakohathi. Walawi wengine, wote kati ya wale waliokuwa wanamziki wazuri sana, kwa ukaribu waliwaelekeza watendakazi. \v 13 Walawi hawa walikuwa viongozi wa wale waliobeba vifaa vya ujenzi na watu wengine wote waliofanya kazi kwa namna yoyote ile. Pia palikuwa na Walawi ambao walikuwa makatibu, watawala na walinda lango.