sw_2ch_text_reg/32/13.txt

1 line
690 B
Plaintext

\v 13 Je, hamjui mimi na babu zangu tulifanya nini kwa makundi ya wote wa inchi zingine? Je, miungu ya watu wa hizo nchi iliweza kwa njia yoyote kuziokoa nchi zao zidi ya nguvu zangu? \v 14 Miongoni mwa miungu yote ya mataifa hayo amabayo babu zangu waliwatekeza, je, kulikuwa na muungu yeyote aliyeweza kuwaokoa watu wake kutoka kwenye mkono wangu? Itakuwaje Mungu wenu aweze kuwakoa ninyi zidi ya nguvu zangu? \v 15 Sasa msimuruhusu Hezekia awadanganye au kuwashawishi katika njia hii. Msimwamini, kwa maana hakuna muungu wa taifa lolote au ufalme amewahi kuwaokoa watu wake nje ya mkono wangu, au nje ya mkono wa babu zangu. Sembuse na Mungu wenu kwa namna gani atawaokoa na mkono wangu?