sw_2ch_text_reg/31/17.txt

1 line
651 B
Plaintext

\v 17 Waliwaganya makuhani kwa mujibu wa kumbu kumbu za babu zao, na hivyo hivyo kwa Walawi wenye umri wa miaka ishirini na zaidi, kwa mujibu wa ofisi zao na zamu zao. \v 18 Waliwajumuisha watoto wao wadogo wote, wake zao, wana wao, na binti zao, katika jamii yote, kwa maana walikuwa waaminifu katika kujitunza wenye watakatifu. \v 19 Kwa maana makuhani, uzao wa Haruni, amabao walikuwa katika mashamba ya vijiji wakimilikiwa na miji yao, au katika kila mji, palikuwa na watu walioteuliwa kwa majina kutoa mafungu kwa ajili ya wanaume miongoni mwa makuhani, na kwa wote waliokuwa wameorodheshwa katika kumbukumbu za babu zao kuwa miongoni mwa Walawi.