sw_2ch_text_reg/31/02.txt

1 line
590 B
Plaintext

\v 2 Hezekia akayapanga makundi ya makuhani na Walawi wakajipanaga kwa makundi yao, kila mtu akapangwa katika kazi yake, wote makuhani na Walawi. Aliwapanga wafanye sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani, kuhudumu, kutoa shukrani, na kusifu katika malango ya hekalu la Yahwe. \v 3 Pia akawapanga katika sehemu ya mfalme kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa kutoka katika mali zake, hiyo ni kwa ajili ya, sadaka za kuteketezwa za asubuhi na jioni, na sadaka za kuteketezwa kwa ajili ya siku za Sabato, mwezi mpya, na sikukuu zisizobadilika, kama ilivyokuwa imeandikwa katika sheria ya Yahwe.