sw_2ch_text_reg/28/16.txt

1 line
388 B
Plaintext

\v 16 Wakati huo Mfalme Ahazi akatuma wajumbe kwa wafalme wa Ashuru kuwaomba wamsaidie. \v 17 Kwa maana Waedomu walikuwa wamekuja tena na kuvamia Yuda, wakachukua wafungwa. \v 18 Wafilisti pia wakavamia miji ya nchi ya chini na ya Negebu ya Yuda. Waliichukua Beth-shemeshi, Ayaloni, Giderothi, SoKo pamoja na vijiji vyake, Timna pamoja na vijiji vyake. Wakaenda kuishi katika sehemu hizo.