sw_2ch_text_reg/26/09.txt

1 line
435 B
Plaintext

\v 9 Zaidi ya hayo, Uzia akajenga minara katika Yerusalemu katika kona ya Lango, kwenye Lango la Bonde, na pa kwenye kona ya ukuta, na akavizungushia ngome. \v 10 Akajenga minara ya ulinzi katika nyika na akachimba mabwawa, kwa maana alikuwa na ng'ombe wengi, katika visiwa vya chini na katika nchi tambarare. Alikuwa na wakulima na wapandaji wa zabibu katika mwinuko wa nchi na katika mashamba yenye rutuba, kwa maana alipenda kulima.