sw_2ch_text_reg/23/18.txt

1 line
434 B
Plaintext

\v 18 Yehoyada akateua wakuu kwa ajili ya nyumba ya Yahwe chini ya mkono wa makuhani, ambao walikuwa Walawi, ambao Daudi alikuwa amewapanga kwenye nyumba ya Yahwe, ili wamtolee Yahwe sadaka za kuteketezwa, kama ilivyoandikwa katika sheria ya Musa, pamoja na kushangilia na kuimba, kama alivyotoa maelekezo Daudi. \v 19 Yehoyada akaweka walinzi katika malango ya nyumba ya Yahwe, ili kwamba kwa namna yoyote ile asiingie mtu asiyesafi.