sw_2ch_text_reg/23/01.txt

1 line
559 B
Plaintext

\v 1 Katika mwaka wa sa saba, Yehoyada alionesha nguvu zake na akaingia katika agano na maakida wa mamia, Azaria mwana wa Yerohamu, Ishmaeli mwana wa Yehohanani, Azaria mwana wa Obedi, Maaseya mwana wa Adaya, na Elishafati mwana wa Zikri. \v 2 Wakaenda katika Yuda na kuwakusanya Walawi kutoka miji yote ya Yuda, vile vile na wakuu wa nyumba za mababu wa Israeli, na wakaja hadi Yerusalemu. \v 3 Kusanyiko lote wakafanya aganao na mfalme katika nyumba ya Mungu. Yehoyada akawaambia, "Ona, mwana wa mfalme atatawala, kama Yahwe alivyosema kuhusu uzao wa Daudi.