sw_2ch_text_reg/22/04.txt

1 line
387 B
Plaintext

\v 4 Ahazia alifanya yaliyokuwa maovu katika macho ya Yahwe, kama nyumba ya Ahabu walivyokuwa wakifanya, kwa maana walikuwa washauri wake baada ya kifo cha baba yake, hadi kuangamia kwake. \v 5 Pia aliufuata ushauri wao; akaenda pamoja na Yoramu mwana wa Ahabu, mfalme wa Israeli, kwa ajili ya kupigana dhidi ya Hazaeli, mfalme wa Aramu, huko Ramothi-gileadi. Waaramu wakamjeruhi Yoramu.