sw_2ch_text_reg/21/01.txt

1 line
514 B
Plaintext

\v 1 Yehoshafati akalala pamoja na babu zake na akizikwa pamoaja nao katika mji wa Daudi; \v 2 Yehoramu, mwanaye, akawa mfalme katika nafasi yake. Yehoramu alikuwa na ndugu, wana wa Yehoshafati: Azaria, Yerieli, Zekaria, Azaria, Mikaeli, na Shefatia. Wote hawa walikuwa wana wa Yehoshafati, mfalme wa Israeli. \v 3 Baba yao alikuwa amewapa zawadi kubwa ya fedha, dhahabu, na vitu vingine vya thamani, na miji yenye ngome katika Yuda, lakini kiti cha enzi alimpa Yehoramu, kwa sababu alikuwa mzaliwa wake wa kwanza.