sw_2ch_text_reg/18/33.txt

1 line
416 B
Plaintext

\v 33 Lakini mtu mmoja akauvuta upinde wake kwa kubahatisha na kumpiga mfalme wa Israeli kati kati ya maungio ya mavazi yake. Kisha Ahabu akamwambia dereva wa gari lake, "Geuza nyuma na nitoe nje ya mapigano, kwa maana nimejeruhiwa vibaya sana." \v 34 Mapigano yakazidi kuwa makali siku hiyo, na mfalme wa israeli akashikiliwa katika gari lake kuwaelekea Waaramu hadi jioni. Muda jua lilipokaria kwenda chini, akafa.