sw_2ch_text_reg/18/09.txt

1 line
535 B
Plaintext

\v 9 Sasa Ahabu mfalme wa Israeli na Yehoshafati mfalme wa Yuda walikuwa wamekaa kila mmoja katika kiti cha enzi, wamevalia kanzu zao, katika sehemu ya uwazi katika maingilia ya lango la Samaria, na manabii wote walikuwa wakitabairi mbele zao. \v 10 Zedekia mwana wa Kenaani akajitengenezea pembe za chuma na kusema, Yahwe anasema hivi: Kwa kutumia hizi pembe mtawasukuma Waaramu hadi waangamie." \v 11 Manabii wote wakatabiri kitu kile kile, wakisema, "Vamia Raamothi-gleadi na shinda. kwa maana Yahwe ameutia kwenye mkono wa mfalme."