sw_2ch_text_reg/16/02.txt

1 line
402 B
Plaintext

\v 2 Kisha Asa akaitoa fedha na dhahabu nje ya vyumba vya kuhifadhia katika nyumba ya Yahwe na nje ya nyumba ya mfalme, na akaituma kwa Ben Hadadi mfalme wa Aramu, ambaye aliishi Dameski. Akasema, pawe na agano kati yako na mimi, kama palivyokuwa na agano kati ya baba yangu na baba yako. Angalia, nimekutumia fedha na dhahabu. \v 3 Livunje agano lako na Baasha, mfalme wa Israeli, ili kwamba aniache."