sw_2ch_text_reg/13/19.txt

1 line
500 B
Plaintext

\v 19 \v 20 \v 21 \v 22 Abiya akamshawishi Yeroboamu; akachukua miji kutoka kwake; Betheli pamoja na vijiji vyake, Yeshana pamoja na vijiji vyake, na Efroni pamoja na vijiji vyake. Yeroboamu hakupata nguvu tena katika siku za Abiya; Yahwe akampiga, na akafa. Lakini Abiya akawa na nguvu sana; akachukua wanawake kumi na nne kwa ajili yake na akawa baba wa wana ishirini na mbili na mabinti kumi na sita. Matendo ya Abiya yaliyosalia, tabia yake na maneno yake yameeandikwa katika kamusi ya nabii Ido.