sw_2ch_text_reg/07/08.txt

1 line
498 B
Plaintext

\v 8 Kwa hiyo Sulemani akaitisha sikukuu wakati huo kwa siku saba, na Israeli wote pamoja naye, kusanyiko kubwa, kutoka Lebo Hamathi mpaka kijito cha Misiri. \v 9 Siku ya nane wakaitisha kusanyiko la makini, kwa maana kwa siku saba walishika kuwekwa wakfu kwa ile madhabahu. \v 10 Katika siku ya ishini na tatu ya mwezi wa saba, Sulemani akawatanya watu kwenda kwenye nyumba zao kwa furaha na mioyo ya shangwe kwa sababu ya wema aliokuwa ameuonesha Yahwe kwa Daudi, Sulemani, Israeli, na watu wake.