sw_2ch_text_reg/05/13.txt

1 line
483 B
Plaintext

\v 13 \v 14 Ikawa kwamba wapuruza tarumbeta na waimbaji wakafanya mziki pamoja, wakifanya sauti moja isikike kwa ajili ya kumsifu na kumshukuru Yahwe. Walipaza sauti zao kwa tarumbeta, toazi na vyombo vingine, na wakamsifu Yahwe. Wakaimba, "Kwa maana Yeye ni mwema, kwa kuwa uaminifu wa agano lake wadumu milele." Kisha nyumba, ile nyumba ya Yahwe, ikajawa na wingu. Makuhani hawakuweza kusimama ili wahudumu kwa sababu ya lile wingu, kwa maana utukufu wa Yahwe uliijaza nyumba yake.