sw_2ch_text_reg/05/11.txt

1 line
472 B
Plaintext

\v 11 Ilikuwa makuhani walipotoka nje ya sehemu takatifu. Makuhani wote waliokuwepo wakajiweka wakfu wenyewe kwa Yahwe, bila kujiamuru wenyewe kulingana na sehemu zao. \v 12 Pia makuhani waliokuwa waimbaji, wote kwa ujumla wao, pamoja na Asafu, Hemani, Yeduthuni, na wana wao na ndugu zao, wakiwa wamevalia kitani safi na wakipiga matoazi, vinanda, na vinubi, wakasimama upande wa mashariki wa mwisho wa madhabahu. Pamoja nao palikuwa na makuhani 120 wakipuliza tarumbeta.