sw_2ch_text_reg/04/11.txt

1 line
522 B
Plaintext

\v 11 Huramu akayatengeza masufuria, majembe, na mabakuli ya kunyunyizia. Hivyo Huramu akamaliza kazi aliyofanya kwa ajili ya mfalme Sulemani katika nyumba ya Mungu: \v 12 zile nguzo mbili, taji mfano wa upinde zilizo kuwa juu ya zile nguzo mbili, na nyavu mbili za mapambo zilizofunika zile taji mbili mfano wa upinde zilizokuwa juu ya zile nguzo. \v 13 Alikuwa ametengeneza makomamanga mia nne kwa ajili ya zile nyavu za mapambo: safu mbili za makomamanga kwa kila wavu ili kufunika vimbe mbili zilizo kuwa juu ya nguzo.