sw_2ch_text_reg/03/10.txt

1 line
583 B
Plaintext

\v 10 Akachonga makerubi wawili kwa ajili ya sehemu za patakatifu pa patakatifu, wahunzi wakayafunika kwa dhahabu. (Maandishi ya kale yanasema: makerubi wawili waliochongwa kwenye mbao). \v 11 Mabawa ya makerubi yalikuwa na urefu wa mikono ishirini yote kwa pamoja; bawa la kerubi mmoja lilikuwa na urefu wa mikono mitano, lilifikia kwenye ukuta wa chumba; bawa jingine lilikuwa na urefu wa mikono mitano pia. \v 12 Bawa la kerubi mwingine lilikuwa mikono mitano, likifikia kwenye ukuta wa chumba; bawa lake jingine lilikuwa mikono mitano pia, likigusana na bawa la kerubi wa kwanza.