sw_2ch_text_reg/02/11.txt

1 line
407 B
Plaintext

\v 11 Kisha Hiramu, mfalme wa Tiro, akajibu kwa maandishi, ambayo alimtumia Sulemani: "Kwa kuwa Yahwe anawapenda watu wake, amekufanya kuwa mfalme juu yao." \v 12 Zaidi ya hayo, Hiramu akasema, "Abarikiwe Yahwe, Mungu wa Israeli, aliyeziumba mbingu na dunia, amempa Daudi mwana mwenye hekima, mwenye karama ya busara na uelewa, ambaye atajenga nyumba kwa aajili ya Yahwe, na nyumba kwa ajili ya ufalme wake.