sw_2ch_text_reg/01/02.txt

1 line
724 B
Plaintext

\v 2 Sulemani akasema kwa Israleli wote, na maakida wa maelfu na wa mamia, na kwa waamuzi, na kwa kila mfalme kiongozi katika Israeli yote, wakuu wa kaya. \v 3 Hivyo Sulemani na kusanyiko lote wakaenda pamoja naye sehemu ya juu iliyokuwa Gibeoni, maana ndipo palikuwepo hema ya kukutania ya Mungu, ambayo Musa mtumishi wa Yahwe, alikuwa ameitengeneza jangwani. \v 4 Lakini Daudi alikuwa ameleta pale sanduku la Mungu kutoka Kiriath yeriam hadi sehemu ambayo alikuwa ametayarisha, maana alikuwa ameliandalia hema huko katika Yerusalemu. \v 5 Zaidi ya hayo, madhabahu ya shaba iliyotengenezwa na Bezaleli mwana wa uri mwana wa Huri ilikuwepo huko kabla ya mbele ya madhabahu ya Yahwe; Sulemani na kusanyiko wakaenda ilikokuwa.