\v 18 Katika mambo mengine kuhusu Manase, maombi yake kwa Mungu wake, na maneno ya waonaji ambao walisema kwake katika jina la Yahwe, Mungu wa Israeli, tazama, yameandikwa miongoni mwa matendo ya wafalme wa Israeli. \v 19 Katika matukio hayo kuna historia ya maombi yake, na jinsi Mungu alivyoguswa na maombi hayo. Pia kuna kumbu kumbu ya dhambi zake zote na makosa yake, na sehemu ambako alikuwa amejenga sehemu za juu na kuzisimamisha Maashera na sanamu za kuchonga, kambla ya kujinyenyekesha mwenyewe -- na imeandikwa kuhusu hayo katika tarehe ya waonaji. (Maandishi ya kale yanasema hivi, "tarehe ya Hozai," ambayo ni maandishi ya kifungu asili. Lakini matoleo mengi ya kisasa yamesahihisha na kusomeka "tarehe ya waonaj" Pia, matoleo machache ya kisasa yanasema "tarehe ya waonaji".). \v 20 Kwa hiyo Manase akalala na babu zake, na wakamzika katika nyumba yake mwenyewe. Amoni, mwaye, akawa mfalme katika nafasi yake.