\v 1 Malikia wa Sheba aliposikia kuhusu umaarufu wa Selemani, akaja Yerusalemu kumjaribu kwa maswali magumu. Akaja pamoja na msafara mkubwa sana, pamoja na ngamia waliosheheni manukato, dhahabu nyingi, na vito vingi vya thamani. Alipofika kwa \v 2 Selemani, akamwambia yaliyokuwa moyoni mwake. Selemani akamjibu maswaali yake yote; hakuna kitu kilichokuwa kigumu sana kwa Selemani; hakuna swali ambalo hakulijibu.