\v 23 Wapiga upinde wakampiga Mfalme Yosia, na mfalme akawaambia watumishi wake, "Niondoeni hapa, kwa maana nimejeruhiwa vibaya." \v 24 Kwa hiyo watumishi wake wakamtoa nje ya gari, na kumuweka katika gari lake la tahadhari. Wakampeleka Yerusalemu, ambako alikufa. Alizikwa katika makaburi ya babu zake. Yuda wote na Yerusalemu wakamwomboleza.