\v 4 Kwa hiyo mfalme na watu wote wakamtolea Yahwe sadaka Yahwe. \v 5 Mfalme Selemani akatoa sadaka ya ng'ombe ishirini na mbili elfu na kondoo 120, 000 na mbuzi. Kwa hiyo mfalme na watu wote wakaiweka wakifu nyumba ya Mungu. \v 6 Makuhani wakasimama, kila mmoja akasimama mahali pake pa kuhudumu; Walawi pia pamoja na vyombo vya muziki vya Yahwe, ambavyo mfalme Daudi alivitengeza kwa ajili ya kumpa shukrani Yahwe katika nyimbo, "Kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele." Makuhani wote wakapiga matarumbeta mbele yao, na Israeli wote wakasimama.