\v 8 Kwa hiyo mfalme aliamuru, na wakatengeneza kasha na kulileta nje kwenye lango kwenye nyumba ya Yahwe. \v 9 Kisha wakafanya tangazo katika Yuda na Yerusalemu, kwa ajili ya watu kuleta kwa Yahwe kodi aliyoiagiza Musa mtumishi wa Mungu juu ya Israeli jangwani. \v 10 Viongozi wote na watu wote wakafurahia na wakaleta fedha na kuiweka kwenye kasha hadi walipomaliza kulijaza.