\v 12 Kisha Sulemani akatoa sadaka za kuteketezwa kwa Yahwe juu ya madhabahu yake ambayo alikuwa ametengeza mbele ya ukumbi. \v 13 Akatoa sadaka kama ilivyohitaka ratiba ya kila siku; akazitoa, kwa kufuata maelekezo yaliyokuwa katika amri ya Musa, katika siku za Sabato, miezi mipya, na katika siku zilizopangwa mara tatu kila mwaka: Sikukuu ya mikate isiyochachwa, sikukuu ya majuma, na sikuku ya vibanda.