1 line
420 B
Plaintext
1 line
420 B
Plaintext
|
\v 35 Baada ya hayo, Yehoshafati, mfalme wa Yuda, akapatana na Ahazia, mfalme wa Israeli, ambaye alitenda uovu mwingi. \v 36 Akapatana naye kujenga meli za kwenda Tarshishi; Wakazijenga meli hizo huko Esion-geberi. \v 37 Kisha Eliezeli, mwana wa Dadavahu wa Maresha, akatoa unabii juu ya Yehoshafati; akasema, "kwa sababu umepatana na Ahazia, Yahwe ameiharibu miradi yako." Meli zilivunjika ili kwamba zisiweze kusafiri.
|